Mshindi wa shindano la Airtel Trace Star Music 2015, Mayunga Nalimi ‘Mayunga’ amefunguka na kueleza ni kwanini aliamua kuipiga chini ‘Universal Music’ ikiwa ni miezi sita toka asaini nao mkataba.


Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Mayunga amesema kuna sababu kubwa tatu ambazo zilimfanya avunje mkataba na Universal Music.
“Kama ambavyo mashindano yalivyokuwa yanasema, mshindi atakuwa amesainiwa Universal Music. Kwa hiyo nilikuwa under Universal Music na wao ndio walikuwa wahusika wa project yangu na Akon, lakini sasa kilichotokea hawakuweza kufanya hivyo na pia mkataba wangu ulikuwa unasema kila baada ya miezi mitatu Mayunga atatoa wimbo. Kwa hiyo baada ya kutoa wimbo wa ‘Nice Couple’ nilitegemea kwenye mwezi wa kumi au kimi na moja, ningetoa wimbo mwingine lakini haikuwa hivyo. Kwa upande wangu mimi nikaona mbona kama kuna delay nyingi alafu hakuna mwendelezo wowote au ratiba hata taarifa labda kuna huu ukimya lakini kuna kitu ambacho kinatengenezwa,” alisema Mayunga.
“Baada ya kuona hata email hawajibu, nikaanza kuona mbona sioni umuhimu wa kuwa Universal Music. Kwa hiyo mimi ikanibidi nikae na management yangu nikawaambia mimi nahisi natakiwa nitoke Universal Music, kwa sababu sioni faida na naona muziki wangu unashuka,” aliongeza.
Mayunga alisema Trace ambao walikuwa partner kwenye mkataba wake, waliamua kuingia kati sakata lake na Universal Music mpaka akafanikiwa kuvunja nao mkataba.
“Nawashukuru Trace, nao waliingia kati kwa sababu na wao walikuwa partners. Kwa sababu wakati nataka kutoka Universal Music walileta ugumu, ilichukua miezi mitatu, lakini kwa nguvu ya Trace wakakubali kuvunja mkataba, Kwa hiyo baada ya hapo Trace wakaamua kuchukua jukumu la kunisimamia, wakahakikisha nimesafiri kwenda Marekani na kolabo na Akon nimefanya. Bahati nzuri Akon alikuwa yupo tayari ananisubiri mimi tu,” alisema Mayunga.
0 comments:
Post a Comment