Wednesday, 24 May 2017

Picha5: Mwakyembe alivyoipokea Serengeti Boys ikitokea Gabon

Tumu ya Serengeti Boys imewasili salama jijini Dar es Salaam kutoka Gabon ilipokua ikishiriki michuano ya AFCON U17 kabla ya kutolewa kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi B kwa kufungwa na Niger bao 1-0.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe alwaongoza watanzania katika mapokezi hayo kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. J.K Nyerere.
Mwakyembe amewapongeza Serengeti Boys kwa kushiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza na kuwaambia kuondolewa kwao ni mwanzo mpya wa safari ya kuitumikia Ngorongo Horoes.
“Karibuni nyumbani, mmetuwakisha vizuri na kuweka rekodi ya kuwa Tanzania tupo, tukienda kwenye mashindano ya kimataifa hatuendi kama wasindikizaji, tunaenda kama washindani.”
“Tunawategemea nyie ndio mtakua Ngorongoro Heroes, maandalizi yanaanza sasa kuelekea michuano inayokuja ili mwakani mtuwakilishe vizuri.”
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 

MAISHA TM Copyright © 2012 Template Designed by BTDesigner Published..Blogger Templates· Powered by Blogger