
Bunge
liliahirishwa leo asubuhi hadi saa 10 jioni baada ya kuzuia kusomwa
kwa hotuba hiyo kwa madai kwamba, ina maneno yanayohitajika kuondolewa
ili ikidhi matakwa baada ya kupitiwa na Kamati ya Kanuni.
Ndani
ya Hotuba ya Lema kipo kipengelea kinachoelezea sakata la makataba
tata wa Kampuni ya Lugumi ambapo Kamati ya Mambo ya Ndani ilielezwa
suala hilo kutojadiliwa bungeni kwa madai tayari lilikuwa limeanza
kuchunguzwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).
Kipengele kinachohusu mkataba wa Kampuni ya Lugumu kipo kwenye sehemu ya tano inayoeleza Mikataba Tata ya Jeshi la Polisi.
Kwa
muda mrefu mkataba huo uliotolewa na Jeshi la Polisi nchini kwa Kampuni
ya Lugumi Enterprises Ltd wenye thamani ya Sh 37 bilioni umedaiwa kuwa
na harufu ya ufisadi.
Mwaka
2011, kampuni hiyo ilipewa zabuni ya kufunga mashine za alama za vidole
katika vituo vya polisi 108 nchini na kulipwa Sh 34 bilioni kati ya Sh
37 bilioni sawa na asilimia 99 ya malipo yote.
0 comments:
Post a Comment