Katibu
mkuu wizara ya habari,utamduni,sanaa na michezo Prof Elisante Ole
Gabriel akizungumza jambo wakati menejimenti ya wizara hiyo ilipofanya
ziara ili kujifunza mfumo wa usimamizi wa nyaraka kidijitali unavyofanya
kazi katika ofisi za wizara ya ujenzi,uchukuzi na mawasiliano leo
jijini Dar es Salaam.Kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Faustin Kamuzora na Naibu katibu
mkuu wizara ya habari,utamaduni,sanaa na michezo Bi.Nuru Khalfan Mrisho.
Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Faustin Kamuzora
akieleza jambo kwa menejiment kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo walipofika ofisini hapo ili kujifunza mfumo wa usimamizi wa
nyaraka kidijitali.
Watumishi
pamoja na Menejimenti kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Kaimu mkuu wa
masijala ya wazi Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Bi.Bupe
Munisi(wa kwanza mwenye nguo ya njano) jinsi mfumo wa usimamizi wa
nyaraka kidijiti(DMIS) unavyofanya kazi .
…………
Mfumo wa usimamizi wa nyaraka kidijiti utaongeza kasi serikalini na hivyo kuchochea maendeleo chanya katika kila nyanja.
Hayo yamesemwa leo na Katibu mkuu
Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel
wakati wa mafunzo yanayotolewa na Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano kwa Menejimenti ya wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo wakati walipotembelea mfumo wa usimamizi wa nyaraka wa kidijiti.
Alisema pia kuwa mfumo huu una
faida nyingi na ndio ambazo zimeifanya wizara hii kutaka kujifunza ni
pamoja na suala la gharama na kwa kuwa serikali ya awamu ya tano iko
katika jitihada kubwa za kupunguza matumizi na kwa kuwa bajeti ya
shajala ni kubwa katika taasisi nyingi za serikali hivyo mfumo huu wa
kidijiti utasaidia kupunguza garama kwani hapatakuwa na haja ya kutumia
karatasi na hivyo kupunguza gharama kubwa.
Prof Elisante pia aliongeza kuwa
mfumo huu utaongeza usiri wa nyaraka hizi na kwa sasa zitakuwa zinasomwa
na yule tu aliyekusudiwa na kutoa pongezi kwa ofisi ya rais manejimenti
ya umma kwa kuhamasisha matumizi ya mfumo huu kwani ukitumiwa vyema
utakuwa na manufaa sana.
Kwa upande wake Katibu mkuu
wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Faustin Kamuzora alisema
kuwa mfumo huo ulijengwa miaka mitatu iliyopita na unaweza kutumika
katika wizara yeyote kwani una ufanisi mkubwa sana kwani kwa sasa
utaweza kuangalia mafaili gani yameingia kwa mfumo wa kidijitali na
kwa namna hii itapunguza garama na muda kwani hatutakuwa tunatumia
karatasi tena.
Prof.Kamuzora alizitaka Taasisi
na Wizara mbalimbali kuwapa elimu ya kutosha watunza kumbukumbu kwani
wao ndio wahusika wakuu wa kwanza wa mfumo huu na hivyo kuwataka
wahusika kuwapa mafunzo ya kompyuta na kuboresha vifaa kama scanner
maofisini mwao.
Nae mmoja wa watunza kumbukumbu
kutoka wizara Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Felomena Swai alisema
amenufaika na mafunzo hayo na yatawasaidia katika utunzaji wa
kumbukumbu kwani sasa watapeleka barua kwa wakati na kurahisisha
utunzaji wa mafaili.
0 comments:
Post a Comment