Tuesday, 31 May 2016

Pesa ya Madafu ni wimbo wenye sound yangu iliyozoeleka – Jay Moe

Rapper Jay Moe amesema mashabiki wake watarajie ‘sound’ tofauti kwenye wimbo wake ujao uitwao Pesa ya Madafu.13267440_1166823470008599_165160329_n
13267440_1166823470008599_165160329_n
Akiongea na mtangazaji wa Jembe FM, John Jackson aka JJ, rapper huyo mkongwe alisema video ya wimbo huo ilifanyika Afrika Kusini na kuongozwa na Kwetu Studio.
“It’s a new different sound ya Jay Moe sio vile ambavyo watu wameexpect zamani, game imebadilika kwahiyo sikutaka kufanya hivi kwenye single yangu ya kwanza ndio maana tukaona tutoe kwanza Hili Game ambayo iko na ile feeling ya Jay Moe na hardcore rap. Sasa hivi tumeamua tuje tofauti zaidi kama ambayo zamani pia nilikuwa nafanya,” alisema rapper huyo.
Jay Moe ni miongoni mwa rappers wakongwe waliowahi kuwa na hits nyingi zikiwemo Bishoo, Cheza Kwa Step, Mvua na Jua, Story 3, Famous na zingine.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 

MAISHA TM Copyright © 2012 Template Designed by BTDesigner Published..Blogger Templates· Powered by Blogger