April 23 mwaka huu Beyonce aliachia albamu yake ‘Lemonade’ kwa kushtukiza yenye nyimbo kumi lakini kilichowashangaza watu wengi ni baadhi ya mashairi yaliyopo kwenye albamu hiyo yanamtaja Jay Z kuwa aliwahi kumsaliti Queen Bey kwa kutoka na Rachel Roy pamoja na Rita Ora, “Becky with the good hair.”
“This is your final warning / You know I give you life / If you try this s t again / You gon’ lose your wife,” ni baadhi ya mashairi mengine ya Queen Bey yaliyomgusa Jay Z.
Kwa mujibu wa gazeti la New York limeripoti kuwa albamu ya Jay Z na Beyonce imeshakamilika na itaachiwa kwenye mtandao wa Tidal hivi karibuni lakini haijajulikana ni lini wataiachia albamu hiyo huku Beyonce akiwa bado anaendelea na ziara yake ya Formation.
0 comments:
Post a Comment