Klabu ya Azam FC leo imezindua duka lake lililopo Kariakoo jijini Dar es Salaam litakalokuwa linauza vifaa vya michezo original vya timu hiyo.
Hili linaifanya timu ya Azam kuwa ya pili kwa Tanzania kufanya hivyo baada ya timu ya Simba kuwa ya kwanza kufungua duka kama hilo Februari 2 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari dukani hapo, Mkurugenzi Mtendaji wa timu hiyo, Saad Kawemba amesema wameamua kufungua duka hilo kutokana na malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo.
“Tumeamua kufungua duka letu la vifaa vya michezo na jezi za klabu yetu kwaajili ya mashabiki wetu. Duka hili la kisasa pia limezingatia mahitaji yote kwani kuna hadi jezi za watoto,” aliongeza.
Aidha duka hilo litakuwa linauza jezi za timu hiyo za marika yote, mipira, skafu, kofia, mabegi makubwa na madogo na vifaa vingine vya michezo.
0 comments:
Post a Comment