Serikali ya Marekani kupitia ofisi ya rais Donald Trump imetangaza kupatia Tanzania ufadhili wa kukabilana na virisu vya ukimwi.
Marekani,
ambayo siku chache zilizopita ilitangaza kusimamisha ufadhili wake kwa
wizara ya afya nchini Kenya, imeipa Tanzania kitita cha dola milioni
526.
Kitita hicho kutoka mfuko wa PEPFAR, kitatumika kufanikisha
mpango wa kutoa huduma kwa zaidi ya watu milioni 1.2 wanaoishi na virusi
hivyo.
Akizungumza baada ya tangazo hilo, mwakilishi wa ubalozi
wa Marekani nchini Tanzania, Virginia Blaser amesema kuwa wanalenga
kufanikisha kizazi kilicho huru kutoka virusi nchini Tanzania.
''Kwa
niaba ya raia wa Marekani, tunafurahia ushirikiano wetu na Tanzania na
tunajitahidi kuhakikisha hakuna anyeachwa nje," Alisema.
- Marekani yasitisha msaada kwa sekta ya afya Kenya
- Tohara ya Wanaume kuzuia Ukimwi Tanzania
Miongoni mwa huduma hizo ni matibabu, ukaguzi, na kuzuia
maambukizi mapya ya virusi hivyo kuanzia sasa hadi Septemba mwaka ujao.
Halikadhalika,
serikali ya Marekani itashirikiana na serikali ya Tanzania kutekeleza
huduma za kuwapima raia milioni 8.6 ili kuwawezesha kujua hali yao ya
virusi.
Pesa hizo pia zitatumika kuimarisha maisha ya wajane na
mayatima wa viurusi hivyo, kuzuia dhulma za kijinsia, pamoja na
kuwafikia zaidi ya watu laki tatu walioambukizwa.
Mashirika
mbalimbali yanayoendesha miradi mbalimbali ya afya nchini Tanzania, kama
vile (TACAIDS), na wakfu wa rais mstaafu, Benjamin Mkapa (Benjamin
Mkapa HIV/AIDS Foundation (BMAF)) yanatarajiwa kushiriki kufanikisha
mpango huo.
Mapema mwezi huu, Marekani ilikatiza ufadhili wake wa
miradi kama hivyo nchini Kenya pamoja na kuyazuia mashirika dhidi ya
kufanikisha miradi yoyote na wizara ya afya ya taifa hilo kutokana na
usimamizi mbaya wa fedha.
0 comments:
Post a Comment