Mshambulizi
wa Yanga, Malimi Busungu, amefunguka mambo mawili makuu ambayo ikitokea
siku ameondoka ndani ya timu hiyo basi hawezi kuyasahau popote pale
aendapo.
Busungu
ambaye kwa muda mrefu amepoteza nafasi ya kucheza kwenye kikosi hicho
tangu kinanolewa na Mholanzi, Hans van Der Pluijm kisha Mzambia, George
Lwandamina, mkataba wake na Yanga unamalizika mwishoni mwa msimu huu.
Mshambuliaji
huyo ambaye alijiunga na Yanga msimu wa 2015/16 akitokea Mgambo JKT,
amefanya mahojiano maalum na kipindi cha SPOTI HAUSI kinachorushwa na
Global TV Online kila Alhamisi, na kuyataja mambo hayo.
“Kwanza
kabisa siku nikiondoka Yanga, kwa yale mazuri sitasahau jinsi mashabiki
walivyonipokea wakati najiunga na timu hii, kwa kweli walinipokea
vizuri.
“Lakini
katika jambo ambalo sipendezwi nalo ndani ya Yanga, ni kitendo cha
benchi la ufundi kuamua kumtumia mchezaji mgonjwa na kumuacha mzima nje,
kitu hicho huwa hakinifurahishi hata kidogo, imenitokea sana hiyo na
nimekuwa mkimya tu kwa sababu siku zote mtu akinikwaza namuacha sitaki
na yeye nimkwaze,” alisema Busungu.
0 comments:
Post a Comment