Thursday, 18 May 2017

Rushwa yafifiza vita dhidi ya Boko Haram

Shirika la kimataifa la kupambana na rushwa Transparency International limesema rushwa kwenye jeshi la Nigeria inafifisha juhudi za kupambana na wapiganaji wa Boko Haram.
Shirika hilo linawashutumu maafisa kwa kutengeneza mikataba bandia ambapo wamekuwa wakiiba pesa kwa madai ya kununua vifaa muhimu.
Ripoti hiyo imesema hali hiyo imelifanya Jeshi kuwa na rasimali pungufu pamoja na kutokakuwa na mafunzo ya kutosha.
Msemaji wa Jeshi la Nigeria Meja Jenerali John Enenche amesema tuhuma hizo haziwahusu maafisa wa sasa Jeshi.
Amesema hatua kubwa zimefanyika kuboresha mafunzo na kuinua ari kwa vikosi vya jeshi.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 

MAISHA TM Copyright © 2012 Template Designed by BTDesigner Published..Blogger Templates· Powered by Blogger