katika Mechi za Copa America ambazo zilikuwa zinapigwa usiku wa kuamkia leo matokeo ni kuwa Haiti wamepigwa bao moja kwa sifuri na Peru, Brazil na Equador wakatoshana nguvu ya bila bila huku Venezuela wakiwaonyesha Jamaica kuwa Soka siyo muziki wa Rege kwa kuwabamiza bao moja kwa sifuri.
This is default featured slide 1 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 2 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 3 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 4 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
This is default featured slide 5 title
Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.
Home » Archives for June 2016
Monday, 6 June 2016
Jamie Vardy kutua Arsenal ?
Kijana wa miaka 29 Jamie Vardy kutoka Leicister City anatarajiwa hii leo kutoa majibu iwapo atajiunga na Club ya Arsenal kabla hajaelekea kwenye michuano ya Euro za mwaka huu akiwa na timu ya taifa la Uingereza.Arsenal tayari wamefikia makubaliano na Leicester na wamemwekea mezani Vardy kitita cha fedha kwa miaka minne.
Vardy bado alikuwa anatafakari kama awaache Mbweha kuelekea kwa washika Bunduki. Itakumbukwa Vardy aliisaidia sana Leicister katika kutwaa taji la Ligi kuu akifunga mabao 24.
Andy Murray ahitaji mapumziko zaidi
Katika Tenisi Andy Murray amesema angependa kuyapa kipaumbele mapumziko katika kuelekea Wimbledon baada ya kupokea kipigo kutoka kwa Novak Djokovic katika French Open.
Hili ni taji la kwanza la French Open kwa Mserbia Djokovic na anakuwa mtu wa kwanza wa kizazi hiki kuwa na rekodi ya kuwa na Grand Slams nne kwa wakati mmoja. Mara ya mwishi rekodi ya namna hiyo alikuwa nayo Rod Laver mwaka 1969
Marekani kuipa TZ msaada wa dola 800m
STATEHOUSE TANZANIA
Uhusiano kati ya Marekani na Tanzania unaonesha dalili za kuimarika licha ya nchi hiyo kukatiza msaada wa awamu ya pili ya mradi wa changamoto za milenia (MCC-2) kwa Tanzania.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mheshimiwa Mark Childress amesema hayo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Bwana Childress alisema kuwa hivi karibuni ''kupitia shirika la misaada la Marekani, USAID tunatarajia kutia saini mkataba wa zaidi ya dola milioni 400 kwa ajili ya mwaka ujao.
''Aidha tumezungumza kuwa kutakuwa na dola milioni 800 zitakazotolewa na Marekani kwa ajili ya miradi mbalimbali na hii haihusiani na MCC.'' Alisema balozi Childress
"Ukweli ni kwamba tunayo mengi ya kufanya pamoja katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu na kilimo na tutafanya kila juhudi kuhakikisha yanafanikiwa"
Rais Magufuli kwa upande wake alisema kuwa serikali yake itaendeleza kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano na Marekani.
Aidha rais huyo alisema kwamba fedha za msaada kutoka Marekani ni muhimu kwa maendeleo ya Tanzania.
"Amekuja kutuhakikishia kwamba watatoa hela kwa ajili ya Tanzania na anasema sasa hivi watatoa zaidi ya dola milioni 800, na mkataba mwingine tunaweza tukasaini hata kesho wa dola milioni 410.
Rais Magufuli alisema ''Balozi anasema kutotoa hela za MCC hakuna maana kupotea kwa urafiki wa Tanzania na Marekani, urafiki wa Tanzania na Marekani upo pale pale na sasa wanaongeza hela nyingi zaidi katika kuonesha kwamba juhudi za ''Hapa kazi tu'' zinaendelea" Taarifa hiyo ya ikulu ilielezea.
Polisi Jijini Mwanza Wapambana na Majambazi kwa Saa 16.....Wakamata Silaha Nzito, Watatu Wauawa
Watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi,wameuawa katika majibizano ya risasi na askari polisi mkoani Mwanza,alfajiri ya kuamkiajana jumapili katika mapango ya mlima wa Utemini yaliyopo kata ya Mkolani jijini Mwanza.
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Ahmed Msangi,amewataja majambazi waliouwa katika majibizano ya risasi usiku kucha kuwa ni Omar Francis Kitaleti mkazi wa Nyegezi Kona,said Khamis Mbuli maarufu kama fundi bomba mkazi wa bugarika na jambazi mwingine ambaye jina lake bado halijafahamika.
Amesema majambazi hayo yalikuwa yamejificha kwenye mapango ya mlima wa Utemini kabla ya askari polisi kufanikiwa kuyaua.
Jambazi mmoja aliyeuawa ambaye hajafahamika jina lake mwenye umri kati ya miaka 20 hadi 25 alikuwa akiwashambulia polisi kwa kutumia bastola ambapo baada ya polisi kumpiga risasi walimpekua na kumkuta akiwa na bastola aina ya Chinese,iliyokuwa na risasi tatu ndani ya magazine,huku majambazi wengine waliokuwepo kwenye mapango hayo wakiendelea kujibishana kwa risasi na askari polisi.
Kamanda Msangi ameongeza kwamba Ijumaa Juni 3,askari polisi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama,walimkamata Omar Francis Kitaleti kwa jina maarufu kiberiti,mkazi wa Nyegezi Kijiweni ambaye alikuwa akituhumiwa kuhusika katika matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha kwenye maduka ya M-pesa,Tigo Pesa na Airtel money jijini Mwanza ambaye baada ya kuhojiwa alikiri kuhusika katika matukio hayo na aliwataja wenzake anaoshirikiana nao na mahali walipojificha.
Amesema ilipotimu majira ya saa kumi na moja kamili jioni siku ya Jumamosi Juni 4,polisi walifika katika mlima huo na walipoyakaribia mapango hayo ghafla walianza kushambuliwa kwa risasi na majambazi waliokuwa wamejificha ndani ya mapango hayo.
Omary Francis Kitaleti @Kiberiti, mmoja wa majambazi aliyeuawa na wenzake kwa risasi.
Katika mapambano hayo ya risasi na askari polisi,risasi hizo ziliweza kumpata jambazi mwenzao aitwaye Omary Francis Kitaleti aliyekuwa anawaongoza askari polisi na kufariki dunia papo hapo, na risasi nyingine ilimjeruhi askari kwenye unyayo wa mguu wake wa kulia.
Amesema polisi kwa kutumia mbinu za medani za kivita waliweza kuzingira maeneo hayo ya mlima wa utemini hadi alfajiri ya kuamkia Jumapili Juni 5,huku wakijibishana risasi na majambazi hao na baada ya kuona yamezidiwa nguvu huku kukikaribia kupambazuka ndipo yalipoamua kuondoka ndani ya mapango hayo kwa kurusha bomu moja la kutupa kwa mkono huku yakizidisha mapigo ya risasi kwa kutumia silaha walizokuwa nazo.
Ameongeza kuwa polisi wamekamata bunduki moja aina ya SMG iliyokuwa na risasi nane na kisu kimoja.
Kamanda Msangi amesema majambazi watatu walifanikiwa kutoroka kutoka kwenye mapango hayo kuelekea maeneo ya Nyasaka na baada ya jambazi mmoja kubaini kuwa askari polisi walikua wanamfuatilia alitoa bunduki na kutaka kuwapiga askari polisi lakini polisi waliweza kumuwahi na kumfyatulia risasi sehemu mbalimbali za mwili wake na kufariki dunia papo hapo.
Amesema askari polisi wamefanya upekuzi kwenye mapango ya mlima wa Utemini na kufanikiwa kupata vitu mbalimbali vilivyoachwa na majambazi hao ambavyo ni pamoja na risasi nne,kisu kimoja chenye damu,kofia ya kuficha uso nyeusi moja (mask),jiko la stove,masufuria ya kupikia, unga wa mahindi,sukari,dagaa,chakula kilichopikwa,ngoma mbalimbali,na simu tatu za mkononi.
Askari aliyejeruhiwa amelazwa hospitali ya rufaa ya bugando na hali yake inaendelea vizuri,polisi bado wanaendelea na msako wa kuwatafuta majambazi waliofanikiwa kutoroka.
Askari aliyejeruhiwa amelazwa hospitali ya rufaa ya bugando na hali yake inaendelea vizuri,polisi bado wanaendelea na msako wa kuwatafuta majambazi waliofanikiwa kutoroka.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo alitembelea kwenye mapango ya Utemini na kuwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi katika kuwafichua wahalifu
Jinsi Punyeto Inavyo Sababisha Ukosefu Na Upungufu Wa Nguvu za Kiume
Ukosefu na/ama upungufu wa nguvu za kiume, ni tatizo linalo wakabili mamilioni ya wanaume duniani. Zipo sababu nyingi zinazo sababisha tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume.
Miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na maradhi kisukari, presha,shinikizo la damu, moyo, figo, matatizo kwenye mishipa ya ubongo & mishipa ya uti wa mgongo, matatizo kwenye mishipa itumikayo kusafrisha damu mwilini, maradhi ya ngiri, pamoja na upigaji punyeto kwa muda mrefu.
Katika makala yetu ya leo, tutaangalia namna suala la upigaji punyeto linavyo athiri nguvu za kiume.
Kabla hatujaangalia namna suala la upigaji punyeto linavyo maliza nguvu za kiume, ni vyema tukafahamu kwanza kuhusu SAYANSI YA MFUMO WA NGUVU ZA KIUME.
Kufahamu kuhusu SAYANSI YA MFUMO WA NGUVU ZA KIUME tafadhali tembelea :
Ukisoma vizuri kuhusu mfumo wa nguvu za kiume, utagundua kuwa Suala la nguvu za kiume ni suala la kimfumo. Ili mwanaume awe na nguvu za kiume, aendelee kuwa na nguvu za kiume na azilinde nguvu zake za kiume, ni lazima ogani zote zinazo husika na mfumo wa nguvu za kiume ziwe na afya njema na ziwe na ushirikiano thabiti na wenye afya.
Vile vile , utagundua kuwa , mambo makuu muhimu katika mfumo wa nguvu za kiume ni kama ifuatavyo:
i.Mishipa imara ya ubongo na yenye afya njema
ii. Mishipa imara ya uti wa mgongo ( spinal cords )
iii.Mishipa imara itumikayo kusafirisha damu mwilini ( Blood Vessels )
iv. Mfumo imara wa usafirishaji damu mwilini
v. Mishipa ya uume iliyo imara na yenye afya njema
vi. Uhusiano imara na wenye afya kati ya mishipa ya fahamu iliyopo katika ubongo, mishipa ya kwenye uti wa mgongo pamoja na misuli & mishipa ya kwenye uume.
Hivyo basi, ili mwanaume aweze kuwa na nguvu imara za kiume, na aendelee kuwa na nguvu hizo ni lazima mambo yote muhimu katika mfumo wa nguvu za kiume yawe imara pasi na hitilafu yoyote.
Hitilafu yoyote katika mambo hayo, itasababisha ukosefu na/ama upungufu wa nguvu za kiume kwa mwanaume huyo. Pale inapotokea hitilafu ama mapungufu katika ogani zaidi ya moja kati ya zilizo tajwa hapo juu, basi tatizo kwa muhusika huwa kubwa mara dufu.
JINSI PUNYETO INAVYO SABABISHA TATIZO LA UKOSEFU & UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.
Mwanaume anapopatwa na wazo la kufanya tendo la ndoa, ubongo hutoa ishara kwenye mishipa ya uti wa mgongo ambayo nayo husafirisha taarifa hadi kwenye mishipa & misuli ya uume.
Mishipa ya uume inapopokea taarifa hiyo, hutanuka. Na mishipa ya uume inapotanuka, hufanya mambo mawili muhimu sana :
i.Husababisha mishipa ya ateri kupanuka na hivyo kuruhusu damu kuingia kwa kasi sana ndani ya mishipa ya uume na hivyo kuufanya uume usimame na kuwa imara bara bara.
ii. Huibinya na kuiziba mishipa ya vena na hivyo kuzuia kunyonya ama kufyonza damu iliyo ingia ndani ya mishipa ya uume. ( KAZI KUBWA YA MISHIPA YA VENA ILIYO KARIBU NA MISHIPA YA UUME NI KUHAKIKISHA HAKUNA DAMU NDANI YA MISHIPA YA UUME. HIVYO BASI DAMU INAPOINGIA NDANI YA MISHIPA YA UUME, MISHIPA YA VENA HU “SENSE” JAMBO HILO KWA HARAKA NA HIVYO KUIFYONZA DAMU HIYO KUTOKA KWENYE MISHIPA YA UUME YA KUITOA NJE YA MISHIPA YA UUME. NA DAMU INAPOKOSEKANA NDANI YA MISHIPA YA UUME, HUUFANYA UUME KUSINYAA NA KULEGEA )
Mtu anayepiga punyeto husababisha mambo yafuatayo katika mwili wake :
1. Huuwa nguvu ya mishipa & misuli ya uume ambayo ndio inayo husika na kusimama kwa uume
2. Mishipa ya uume inapo sinyaa na kukosa nguvu yake ya asili, husababisha mambo yafuatayo :
i.Huondoa uwezo wa mishipa & misuli ya uume kutanuka, na hii ndio sababu inayo wafanya waathirika wa punyeto kutumia nguvu nyingi sana katika kuufanya uume usimame.
ii.Huondoa uwezo wa mishipa & misuli ya uume kuibana na kuiziba mishipa ya vena, na hii ndio sababu inayo fanya waathirika wa punyeto kufika kileleni haraka sana, kwani damu inayo ingia kwenye misuli ya uume hufyonzwa ndani ya muda mfupi sana.
Hii hutokea kwa sababu mishipa na misuli ya uume inakuwa imelegea,na mishipa ya vena inakuwa imepwaya, hivyo msuguano wowote ule hufanya mishipa ya vena kufunguka na kufyonza damu kutoka kwenye mishipa ya uume na hivyo kuufanya uume kusinyaa ndani ya dakika ama sekunde chache sana.
3. Vile vile punyeto hufanya uume kusinyaa na kurudi ndani na kuufanya uonekane kama uume wa motto mdogo.
Kwa ufupi punyeto husababisha ukosefu wa nguvu za kiume kwa sababu kuu zifuatazo :
i.Kwanza hudhoofisha na kuharibu mishipa ya uume, ambayo ndio hufanya uume kusimama.
ii.Pili hudhoofisha utendaji kazi wa mishipa ya ateri, ambayo ndio hutumika kama njia ya kusafirisha damu kupeleka kwenye misuli ya uume na ivyo kuufanya uume usimame
iii. Tatu, punyeto hupelekea kuvuja kwa mishipa ya vena na hivyo kusababisha damu kufyonzwa kwa haraka sana kila iingiapo ndani ya misuli ya uume na matokeo yake ni uume kusimama kwa muda mfupi sana wakati wa tendo la ndoa.
iv. Punyeto huathiri mtiririko wa damu kwenda kwenye mishipa ya uume, kwa sababu hudhoofisha misuli & mishipa ya uume pamoja na mishipa ya ateri ambayo ndio hutumika katika kusafirisha damu kwenda kwenye uume
DALILI ZA MTU ALIYE ATHIRIWA NA PUNYETO
Dalili kuu za mtu aliye athiriwa na punyeto ni kama ifuatavyo:
i. Uume kusinyaa na kuwa kama wa mtoto
ii. Uume kurudi ndani
iii. Uume kusimama ukiwa legelege
iv. Kufika kileleni haraka wakati wa tendo la ndoa.
TIBA YA NGUVU ZA KIUME KWA MTU ALIYE ATHIRIKA NA PUNYETO.
Dawa asilia ya nguvu za kiume iitwayo JIKO ni tiba bora na ya uhakika kabisa kwa mtu aliye athiriwa na punyeto. Dawa hii, pamoja na mambo mengine mengi, husaidia kufanya mambio yafuatayo katika mwili wa mwanaume aliye athiriwa na punyeto :
i.Kuimarisha mishipa & misuli ya uume ulio legea na hivyo kuurejeshea uwezo wake wa asili
ii. Hutibu tatizo la uume kurudi ndani
iii.Humaliza tatizo la kusimama kwa uume ukiwa legelege
iv.Hutibu na kuponya kabisa tatizo la kufika kieleleni haraka.
BEI YA DAWA : Dawa hii inapatikana kwa gharama ya SHILINGI ELFU THEMANINI TU (Tsh. 80,000/=)
MAHALI INAPOPATIKANA : Dawa hii inapatikana katika duka la dawa asilia liitwalo NEEMA HERBALIST & NUTRITIONAL FOODS CLINIC lililopo jijini DAR ES SALAAM katika eneo la UBUNGO nyuma ya jengo la UBUNGO PLAZA karibu na SHULE YA MSINGI UBUNGO NATIONAL HOUSING.
Kwa wateja wasio weza kufika ofisini kwetu. Watafikishiwa dawa mahali popote walipo jijini DAR ES SALAAM.
Kwa wateja waliopo mikoani watatumiwa dawa kwa njia ya MABASI
Kwa wateja waliopo Zanzibar wata fikishiwa dawa kwa njia ya usafiri wa boti.
Na kwa wateja waliopo UGHAIBUNI watatumiwa dawa kwa njia ya POSTA ama DHL.
MAWASILIANO : WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0766 53 83 84.
Mikataba ya Polisi Yaitishwa Wizarani
BAADA ya Rais John Magufuli kuizungumzia mikataba ya ujenzi ya Jeshi la Polisi iliyoingia na wawekezaji, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ameitisha mikataba yote ya jeshi hilo.
Jeshi la Polisi nchini limetakiwa kuwasilisha mikataba ya miradi ya ujenzi wa nyumba za kuishi askari eneo la Kunduchi, Mikocheni pamoja na Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es Salaam pamoja na ule wa majengo mbalimbali ya mwekezaji ambaye Jeshi la Polisi limeingia mkataba naye.
Agizo hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira ikiwa ni miezi miwili tu tangu Rais Magufuli kuzungumzia mikataba hiyo na kuitilia shaka wakati akifungua kikao kazi cha makamanda wa Polisi wa mikoa, mawakili wafawidhi wa serikali wa mikoa na wakuu wa upelelezi wa mikoa na vikosi mjini Dodoma.
Meja Jenerali Rwegasira alisema mradi huo ni mkubwa na wa muda mrefu na hivyo ameliagiza jeshi hilo kuuwasilisha mkataba huo, ambao utekelezaji wake unaendelea ili aufahamu vizuri mkataba huo, unaolihusisha Jeshi la Polisi na Mwekezaji wa Kampuni ya Mara World Tanzania Limited.
Kwa mujibu wa taarifa ya wizara hiyo jana kwa vyombo vya habari, Katibu Mkuu huyo ametoa agizo hilo muda mfupi baada ya kukagua miradi hiyo katika maeneo ya Kunduchi na Mikocheni, ambako zinajengwa nyumba za kuishi askari wa Jeshi la Polisi na kwamba ujenzi wake bado unaendelea.
Mradi mwingine alioutembelea ni ujenzi wa Kituo cha Polisi eneo la Polisi Oysterbay na kuona maendeleo ya ujenzi huo sambamba na kufahamu hatua iliyofikiwa hadi sasa katika maeneo hayo ya Jeshi la Polisi.
Katika mradi huo wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi Oysterbay, unaotekelezwa na mwekezaji Kampuni ya Mara World Tanzania Limited, pia kutajengwa ofisi za kukodisha, hospitali, maduka makubwa na hoteli.
Rais Magufuli wakati akihutubia makamanda hao wa Polisi Aprili mwaka huu, alisema miongoni mwa vitu ambavyo vinalisumbua jeshi hilo ni mikataba ya hovyo akisisitiza umuhimu wa fedha za jeshi hilo kutumika vizuri.
Rais Magufuli alisema kuna taarifa zinaonesha Jeshi la Polisi, limekuwa likihusishwa na matumizi mabaya ya fedha, hali inayoongeza ukubwa wa matatizo yanayokwamisha utendaji wake wa kazi.
Alitoa mfano wa taarifa za matumizi mabaya ya fedha, zinazotolewa kwa ajili ya kununua vifaa na sare za askari ama mikataba yenye mashaka inayotiwa saini kati ya Polisi na wawekezaji kuwa ni baadhi ya mambo yanayoongeza hali ngumu ya utendaji kazi kwa jeshi hilo.
“Oysterbay pale ni eneo ambalo ni zuri sana, kila mmoja anajua, mmeingia kwenye mikataba mnayoijua ninyi, mkapewa mtu anawajengea pale, sifahamu kama majengo hayo yanafaa.
“Palikuwa na ubaya gani eneo la Oysterbay likawa na hati, mkaitumia hiyo hati kwenda kukopa benki na kujenga nyumba hata za ghorofa 20 pale, mkaweka kitega uchumi na polisi wenu wakakaa pale?
“Nimesema lazima nizungumze kwa uwazi, nisiposema kwa uwazi nitajisikia vibaya nikimaliza mkutano huu. Nataka muelewe na muelewe ukweli mwelekeo ninaoutaka mimi,” alisema Rais Magufuli.
Subscribe to:
Comments (Atom)





























