This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Monday, 26 September 2016

Waziri Mkuu Majaliwa Awasimamisha Kazi Maofisa Misitu Wanne, Apiga ‘stop’ Uvunaji Magogo Rufiji

0 comments

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Maofisa Misitu wanne na kusimamisha shughuli za uvunaji wa mazao ya misitu wilayani Rufiji kwa muda usiojulikana baada ya kutoridhishwa na usimamizi wake.

Maofisa waliosimamishwa kazi ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Dk. Paul Ligonja, Ofisa Misitu wilaya Gaudens Tarimo, Ofisa Misitu Yonas Nyambuya na Ofisa wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) wa wilaya Seleman Bulenga.

Waziri Mkuu amefanya uamuzi huo leo (Jumatatu, Septemba 26, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Rufiji kwenye ukumbi wa halmashauri kabla ya kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye viwanya jumba la maendeleo wilayani Rufiji.

Aidha, Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo, Juma Njwayo kukusanya magogo yoye yaliyoko msituni na kuyapiga mnada na kuitaka  wizara ya Maliasili na Utalii kwenda wilayani Rufiji kufanya uchunguzi wa leseni za uvunaji walizozitoa kwa wilaya hiyo.

Waziri Mkuu amebainisha kwamba wilaya ya Rufiji ni moja kati ya wilaya inayoongoza kwa uvunaji wa mazao ya misitu bila ya kufuata taratibu licha ya kuwa na maofisa misitu.

“Hakuna mafanikio katika sekta ya misitu kwenye wilaya hii ya Rufiji. Nasimamisha shughuli zote za uvunaji wa mazao ya misitu pamoja na watendaji wake kwa sababu hatuwezi kuacha watu wanakata magogo bila ya kufuata taratibu,”

“Haiwezekani Rufiji iwe shamba la bibi, nimesimamisha uvunaji wa magogo hata kwa wenye leseni hadi tuzichunguze zimetoka wapi. Hatuwezi kuruhusu maofisa wanashiriki vitendo vya hujuma kwa kuvuna misitu Rufiji na kugonga mihuli ya Kilwa kisha fedha wanatia mifukoni,” amesema.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo Rashid Salum kufuatilia maagizo aliyoyatoa kuhusu kizuizi cha Ikwiriri kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe alipokutana na watumishi wa wizara hiyo.

Julai 18 mwaka huu Waziri Mkuu alikutana na watumishi wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam  na kusisitiza kwamba hakuna sababu ya Serikali kuendelea kuwa na watumishi wasiokuwa na uaminifu, uadilifu na uwajibikaji.

Waziri Mkuu aliitaka wizara hiyo kupunguza idadi ya vizuizi vya ukaguzi wa mazao ya misitu kwenye  barababara  mbalimbali baada ya kukosa tija, alitoa mfano wa barabara ya kwenda mikoa ya kusini  kuanzia Dar es Salaam yenye vizuizi visivyopungua sita na kila kizuizi kinatumika kwa ajili ya kukagua mazao ya misitu na maliasili inayotoka kuvunwa.

Awali mbunge wa Rufiji Mohammed Mchengelwa alilalamikia vitendo vya dharau vinavyofanywa na watumishi wa sekta mbalimbali katika wilaya hiyo jambo linalosababisha wananchi kukosa imani na Serikali yao. 
Continue Reading...

Thursday, 8 September 2016

Picha: maajabu mapya yaliyoingia kwenye kitabu cha Guinness, yupo paka mkubwa kama mbwa

0 comments
Kama unataka ushangazwe na maajabu ya dunia, basi kitabu cha Guinness World Records hakina mpinzani. Kimesheheni mambo, watu, vitu na vingine vinavyoweza kukuacha mdomo wazi.
3805dcf700000578-3778734-image-a-30_1473318169840
Mwanamke mwenye umri mdogo aliye na ndevu nyingi: Harnaam Kaur wa Uingereza, ana ndevu zenye urefu inchi sita. Ana umri wa miaka 24
Kitabu kipya, toleo la 62 kwaajili ya mwaka 2017 kimetoka kikiwa na maajabu zaidi ya 4,000. Kitabu hicho kimeingia sokoni Alhamis hii na kinauzwa kwa £20. Haya ni baadhi ya maajabu yaliyomo kwenye kitabu hicho kipya.
38013deb00000578-0-image-a-2_1473283649892
Paka mrefu zaidi: Akiwa na urefu wa futi 3ft 10.6in, Ludo anaishi na mmiliki wake Kelsey Gill huko Ryhill, West Yorkshire. Anasema: ‘Ni rafiki wa wote lakini baadhi ya wageni humuogopa sababu wamezoea kuona mbwa mwenye ukubwa kama wake’
miguu
Maxwell Day, 14, anaweza kuizungusha miguu yake kwa nyuzi 157
38018f4d00000578-3778734-image-a-12_1473283911608
Mbwa mwenye mkia mrefu zaidi: Keon ana mkia wenye urefu wa inchi 30.2. Anaishi Ubelgiji
3801693300000578-3778734-image-a-14_1473283984319
Mtu aliyevutwa na farasi umbali mrefu zaidi akiwa amewashwa moto. Josef Todtling wa Austria, alivutwa umbali wa futi 1,640 akiwa amewashwa moto mwili mzima. Alikuwa amevaa nguo nyingi. Ameshikilia rekodi kwa kutumia dakika 4 na sekunde 41
38012e9c00000578-3778734-image-a-16_1473284042338
Domo Kubwa: Bernd Schmidt, 47, wa Wendlingen, Ujerumani anaweza kuufungua mdomo wake kwa upana wa inchi 3.46
3805dcef00000578-3778734-image-a-18_1473284080777
Mabonge ya ice cream yaliyopangwa kwa wiki bila kuanguka. Rekodi hii inashikiliwa na Dimitri Panciera, 54 wa Italia. Alirundika mabonge 121
38013d5f00000578-3778734-image-a-22_1473316335867
Mbwa jike mrefu kuliko wote duniani. Dane Lizzy, ana urefu wa inchi 37.96 na anaishi Alva, Florida, Marekani
3801373800000578-3778734-image-a-28_1473317957447
Mkusanyiko mkubwa zaidi wa vitu vinavyohusiana na hamburger. Harry Sperl (aka Hamburger Harry) kutoka Ujerumani amekusanya vitu 3,724
3801317f00000578-3778734-image-a-44_1473319244969
Mtu mwenye umri mkubwa mwenye tattoo nyingi zaidi: Ms Guttenberg, 67 amejichora asilimia 91.5 yake mwili wake

Chanzo: Mail Online
Continue Reading...

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Akagua makazi yake mapya Dodoma.

0 comments
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu katika eneo la Mlimwa na kuagiza umalizike kwa wakati ili aweze kuhamia kama alivyoahidi.

Katika ziara hiyo aliyoifanya jana mchana (Jumatano, Septemba 7, 2016) Waziri Mkuu alisema ameridhishwa na namna kazi ya ujenzi inavyofanyika.

“Nimekuja kukagua makazi mapya na mahali pa kufanyia kazi. Kazi ya ujenzi inaendelea vizuri, nimejionea mwenyewe na naamini katika kipindi kifupi watakuwa wamekamilisha,” alisema.

Alisema kutokamilika kwa ujenzi huo hauwezi kukwamisha azma yake ya kuhamia Dodoma kwa sababu tayari inafahamika kuwa Makao Makuu ya Ofisi ya Waziri Mkuu yako Dodoma.

Alisema uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma hautokani na shinikizo la kisiasa bali ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao chimbuko lake ni agizo lililotolewa Oktoba Mosi, 1973 kwenye Mkutano Mkuu wa 16 wa chama cha TANU.

“Tangu wakati huo Serikali zote ziliendelea kufanya juhudi mbalimbali za kuandaa miundombinu na hata awamu ya nne ilisimamia kwa kiwango kikubwa uwekaji wa miundombinu hiyo,” alisema.

“Pia tukumbuke kauli ya Mheshimiwa Rais aliyotoa kwenye hotuba yake ya Julai 23, 2016 alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM, na akairudia tena Julai 25, kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa na mimi siku hiyo hiyo nikaweka msisitizo,” alisema.

Alisema uamuzi wa Serikali ya awamu ya tano wa kuhamia Dodoma unakuja baada ya kuridhishwa na ujenzi wa miundombinu na maeneo ya kutolea huduma za kijamii kwa wageni na wenyeji ikiwemo Hospitali ya Benjamini Mkapa iliyopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) yenye uwezo wa kutibu magonjwa makubwa kama ya moyo na figo.

Waziri Mkuu alisema tayari Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) ina mpango kamambe (master plan) na ina viwanja vya kutosha kujenga makazi na ofisi mbalimbali.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU




Continue Reading...

Afariki Kisimani Akimuokoa mbuzi

0 comments
MKAZI wa Kijiji cha Kazibizyo Kata ya Ng’anzo, Wilayani Bukombe, Sebastian Lumbe (36), amefariki dunia kisimani alimoingia   kumuokoa mbuzi kwa ujira wa Sh 6,000.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika Mtaa wa Misheni   baada ya mbuzi huyo kutumbukia kwenye kisima kinachodaiwa kuwa na urefu wa futi 30.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Misheni, Antony Kuya alithibitisha kutokea   tukio hilo.

Alisema baada ya mbuzi huyo kutumbukia kisimani, mmiliki wake, Marco Sylvester alitangaza ujira wa Sh 6,000 kwa mtu ambaye angefanikiwa kumtoa   na ndipo Lumbe alipojitolea kuingia kisimani humo.

Alisema kabla ya Lumbe kuingia kisimani humo na kukutwa na mauti, walijitokeza watu wawili tofauti lakini kila walipoingia waligundua kisima hicho kilikuwa kirefu.

Kwa sababu hiyo  walighairi  hadi alipofika yeye na kujitosa.

“Baada ya kuingia kisimani alianza kupiga kelele za kuomba msaada.

“Watu waliokuwa karibu na kisima hicho walimtupia kamba lakini wakati anajaribu kuivuta kupanda ilikatika na akaanguka kurudi kisimani.

“Baadaye kijana mmoja, Leonard Mathayo aliingia kujaribu kumuokoa lakini wakati akiwa humo ndani alisema baada ya kukaribia kufika mwisho wa shimo alimkuta akitupa miguu.

“Alipoanza kumfunga kamba ili wamvute  aliishiwa nguvu na kukosa hewa na hivyo ilimlazimu kuomba msaada kutoka nje,” alisema Kuya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo aliwaonya wananchi kuwa waangalifu na visima virefu kama hivyo kwa sababu  ni hatari.
Continue Reading...

Tuesday, 6 September 2016

Waziri wa haki Gabon ajiuzulu kupinga matokeo

0 comments


Maandamano GabonImage copyrightAFP/GETTY
Image captionMaandamano yalishuhudiwa baada ya Bw Bongo kutangazwa mshindi
Waziri wa haki nchini Gabon Seraphim Moundounga amejizulu kulalamikia utata ambao umegubika matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika nchini humo wiki moja iliyopita.
Anadaiwa kumuonya Rais Ali Bongo, ambaye alitangazwa mshindi na tume ya uchaguzi, kwamba angefutilia mbali matokeo ya uchaguzi huo iwapo "hayakulingana na uhalisia."
Bw Mondunga ndiye afisa wa juu serikalini kujiuzulu kufuatia mzozo huo kuhusu matokeo ya uchaguzi.
Mamlaka za Gabon zimesema watu watatu wameuawa na zaidi ya 100 kujeruhiwa kwenye ghasia ambapo pia maelfu wamekamatwa.
Baadhi ya taarifa zinasema huenda idadi ya raia waliokufa ikawa juu. Ufaransa imelalamikia hali nchini Gabon na kusema baadhi ya raia wake nchini humo hawajulikani waliko.
Ali Bongo alitangazwa mshindi wa uchaguzi, lakini upinzani ukiongozwa na Jean Ping ulipinga matokeo.
Bw Bongo alipata 49.8% ya kura naye Bw Ping akiwa na 48.2%, tofauti kati yao ikiwa kura 5,594.
Bw Ping alishinda majimbo sita kati ya tisa na ameomba kurudiwa tena kwa shughuli ya hesabu ya kura.
Katika jimbo la Haut-Ogooue, anamotoka Bw Bongo, waliojitokeza kupiga kura walikuwa 99.93% kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na 95% ya kura zilipigiwa rais huyo
Bw Bongo na Bw PingImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionBw Ali Bongo na Bw Jean Ping
Idadi ya wapiga kura waliojitokeza majimbo mengine ni 45% na 71%, kwa mujibu wa wizara ya masuala ya Gabon.
Licha ya Gabon kuwa na utajiri wa mafuta, raia wengi wamesalia masikini
Jean Ping ameomba raia kusalia nyumbani kama mgomo dhidi ya utawala.
Continue Reading...

Tamko Rasmi la Kamati Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo kuhusu Hali ya Nchi kwa Sasa

0 comments

1. Utangulizi

Jana Jumatatu, 5 Septemba 2016, Kamati Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo ilikutana katika kikao chake cha kawaida. Pamoja na mambo mengine, Kamati Kuu ilipokea, kujadili na kuidhinisha Taarifa kuhusu HALI YA NCHI. Taarifa hii sasa inatolewa rasmi kwa umma. Taarifa ipo katika maeneo makubwa manne: Hali ya kisiasa, hali ya kiuchumi, umoja wa kitaifa na hitimisho.

2. Hali ya Kisiasa
Kamati Kuu imezingatia kuwa Kikatiba, nchi yetu inafuata mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Katiba na Sheria mbalimbali zimeanisha utaratibu wa kazi na shughuli za vyama vya siasa. Ili kuhakikisha kwamba kazi na shughuli za vyama vya siasa zinakuwa endelevu, vyama vyenye kukidhi vigezo hupewa ruzuku kupitia Bajeti ya Serikali inayopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania.
 
Hata hivyo, katika awamu hii ya tano, Serikali ya Chama cha Mapinduzi imeamua kuzuia shughuli za siasa kwa kutumia nguvu ya Jeshi la Polisi na hata Jeshi la Wananchi. Kwa mujibu wa serikali ya CCM, shughuli za kiuenezi za vyama vya siasa kama vile mikutano ya hadhara, maandamano, makongamano, mijadala na hata mikutano ya ndani inapaswa kukoma mapema baada ya uchaguzi. 

Kisheria, huu ni uvunjifu wa Katiba na Sheria za nchi. Kisiasa, tunatambua kwamba Viongozi wa CCM wamepoteza mvuto kwa wananchi na sasa wanamsukuma Mwenyekiti wao Rais Magufuli kutumia jeshi katika kuokoa taswira ya Chama cha Mapinduzi mbele ya umma.
 
Kwa kuzingatia hali ya kisiasa nchini kwa sasa, Kamati Kuu ya chama chetu:
i) Tunalaani na kupinga kwa nguvu zetu zote hatua za Serikali ya Chama cha Mapinduzi za kuvunja Katiba na kujaribu kuweka pembeni utawala wa sheria.
ii) Tunapinga vitendo vinavyozidi kushamiri katika serikali hii ya CCM ya kujaribu kuendesha nchi kwa ubabe na matamko ya viongozi badala ya utawala wa sharia.
iii) Tutasimama imara, na tutaungana na vyama vingine vya siasa pamoja na taasisi zingine za kiraia katika kulinda mfumo wa demokrasia ya vyama vingi, uhuru wa maoni, na utawala wa sheria katika nchi yetu

3. Hali ya Kiuchumi​
Katika miaka 10-15 iliyopita, nchi yetu imejenga uchumi ambao umekuwa ukikua kwa kiwango cha asilimia 6-7 kwa mwaka katika kipindi chote hiki. Ukuaji huu wa uchumi ulitokana na juhudi za nchi katika kuvutia wawekezaji na kuchochea shughuli za uzalishaji mali kwa wananchi wenye kipata cha chini. Awamu ya tano ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi imerithi changamoto ya uchumi unaokua bila kuwafaidisha wananchi wa kawaida. Hili ndilo tulitegemea Serikali mpya ishughulike nalo.
 
Kamati Kuu imeshtushwa na hali ya kuanza kudorora kwa shughuli za uchumi katika kipindi cha miezi kumi ya utawala wa awamu ya tano. Kwa mfano:
a) Taarifa za Benki Kuu zilizopo kwenye tovuti yake (Quarterly Economic Review na Monthly Economic Review) kwa robo ya mwisho ya mwaka 2015 (Oktoba - Desemba 2015 ) zinaonesha kuwa kasi ya ukuaji wa Pato la Taifa ilikuwa 9%. Katika robo ya kwanza ya mwaka 2016 (Januari - Machi 2016) kasi ya ukuaji wa Pato la Taifa ilishuka hadi kufikia 5.5%. Kiuchumi, hii inamaanisha kuwa ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika kipindi cha miezi 6 ya mwanzo ya utawala wa awamu ya tano chini ya Rais Magufuli umepungua kwa 4%.
 
b) Shughuli za uchumi zinazohusu wananchi masikini zimeshuka kutoka kasi ya ukuaji ya 10.20% robo ya mwisho ya mwaka 2015 mpaka 2.7% katika robo ya kwanza ya mwaka 2016, ikiwa ni punguzo la 8% ndani ya kipindi kisichozidi miezi sita. Hii ina maanisha kwamba Wananchi wetu wanazidi kudumbukia kwenye ufukara kwa kasi tangu awamu ya tano ya Serikali ya Chama Mapinduzi iingie madarakani
 
c) Ukuaji wa sekta ya ujenzi katika robo ya mwisho ya mwaka 2015 ilikuwa 13.8% lakini ukuaji wa sekta hii katika robo ya kwanza ya mwaka 2016 ilikuwa ni 4.30%, ikiwa ni tofauti ya takribani -10%. Hii ni kwa sababu uwekezaji katika sekta hii umeanza kushuka.
 
d) Kasi ya ukuaji wa sekta ya usafirishaji imeporomoka kutoka kukua kwa 14.50% robo ya mwisho ya 2015 mpaka kukua kwa 7.9% robo ya kwanza ya 2016, ikiwa ni kuporoka kwa 7% katika kipindi cha miezi 6 tu ya kwanza ya utawala wa Rais Magufuli. Kuporomoka kwa sekta ya usafirishaji itaathiri watu wengi, wakiwemo madereva, matingo, pamoja na mama Ntilie wanaowauzia chakula. .
 
Kwa kuzingatia mwenendo wa hali ya uchumi katika nchi, Kamati Kuu:
a) Tunaitaka serikali izingatie sayansi ya uchumi katika kuendesha uchumi wa nchi. Uamuzi wa CCM wa kuitelekeza serikali yake kwa mwanasiasa mmoja anayedhani ndiye anayejua kila kitu na yeye kugeuka kuwa mshauri wa washauri wa uchumi itasambaratisha uwekezaji nchini na kuua kabisa juhudi za miaka 20 za kuvutia wawekezaji na kujenga uchumi shirikishi.

b) Inahimiza wananchi kuzingatia kuwa msingi wa uchumi wetu ni uwekezaji kutoka ndani na nje ya nchi. Msingi wa kuvutia wawekezaji ni utawala wa sheria. Juhudi za serikali ya CCM za kuua utawala wa sheria zitaua uwekezaji na kuangamiza uchumi wa nchi. Tusirihusu CCM iue uchumi wa nchi kwa maslahi yake ya kisiasa na viongozi wake.

4. Umoja wa Kitaifa
Nchi yetu imefanya juhudi kubwa katika miaka 50 iliyopita katika kujenga umoja na mshikamano wa kitaifa kwa kuhakikisha kuwa makabila, dini na baadaye vyama vya siasa tunaishi bila kukamiana. Juhudi za dhati za kupambana na ubaguzi ndiyo umekuwa msingi imara wa kujenga Umoja wa Kitaifa na amani tunayojivunia.
 
Hata hivyo, Kamati Kuu imezingatia kuwa utawala mpya wa Serikali ya CCM, kupitia Mwenyekiti wake mpya na Rais wa Jamhuri wa Muungo, umeanza kwa juhudi na kasi kubwa kuchokonoa na kumomonyoa misingi ya utaifa na umoja wetu. Sasa tunaye Rais asiyechagua maneno na asiyejua aongee nini na wapi. Vijana waliosoma kwa bidii katika mazingira ya shule zilizotelekezwa na serikali ya CCM anawaita VILAZA. 

Katikati ya uhasama mkubwa wa kisiasa na kijamii huko Zanzibar Rais wetu amefunga safari, sio kujaribu kutibu majeraha yaliyosababishwa na kuchezewa kwa sanduku la kura, bali kuchochea uhasama chini ya ulinzi wa vyombo vyetu vya dola vyenye jukumu la kulinda na kudumisha amani. Sasa Rais wetu, kupitia kauli zake, ameanza kuubomoa muungano wetu uliojengwa kwa unyenyekevu na katika mazingira magumu. 

Kila asimamapo kuhutubia, jambo moja la kutarajiwa kutoka katika kinywa cha Rais wetu ni matamshi yanayodhoofisha nguzo fulani ya umoja, mshikamano na undugu wetu kama taifa. Yote haya yakitokea chama chake cha CCM ama kimekaa kimya au kinachekelea. 

Inasikitikitisha kwamba Chama kilichoasisiwa na Mwalimu Nyerere kinamruhusu kiongozi wake kubomoa misingi ya umoja wa kitaifa na kuchochea chuki katika jamii ya watanzania.
 
Kwa kuzingatia mtikisiko mkubwa katika umoja na mshikamano wa kitaifa unaoendelea nchini, Kamati Kuu:
a) Tunalaani juhudi zinazofanywa na Serikali ya CCM kupitia Mwenyekiti wao za kuchochea chuki katika jamii ya watanzania na kubomoa misingi ya umoja wa kitaifa na amani ya nchi
b) Tunatoa wito kwa watanzania wote waipendayo nchi yao kusimama kidete katika kulinda misingi ya nchi yetu na kukataa chuki inayoanza kujengwa na utawala wa CCM
c) Tunatoa wito wa kipekee kwa viongozi wetu wa dini na wakuu wa nchi waliopita, hususani Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mzee Benjamin Mkapa na Mzee Jakaya Mrisho Kikwete, pamoja na wazee wengine wanaoheshimika katika nchi yetu wavae ujasiri wa kumuonya Mwenyekiti wa CCM kuwa juhudi zake za kuchochea chuki katika jamii yetu ya watanzania zitasambaratisha Taifa letu.

5. Hitimisho

i) Sisi kama chama cha siasa, tunaendelea kusisitiza kuwa tutaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kupambana na ufisadi na kujenga uwajibikaji nchini.
ii) Tunaamini kwa dhati kabisa kuwa kuheshimu na kulinda demokrasia na kuzingatia utawala wa sheria nidyo msingi wa mapambano dhidi ya ufisadi. Tunasisitiza kuwa mtu yeyote, wa kawaida au kiongozi, anayesema kwamba anaweza akapambana na ufisadi kwa kukanyaga misingi ya demokrasia na utawala wa sheria mtu huyo ni mwomgo na kwa kweli ni fisadi na anataka kujenga himaya mpya ya ufisadi. Mtu huyo, pamoja na mambo yake yote, yafaa akataliwe na kudharauliwa haraka!
 
iii) Tunasisitiza kuwa msingi wa uchumi wetu ni kuvutia uwekezaji wa ndani nan je ya nchi. Kuzingatia utawala wa sheria ndiyo msingi wa kuvutia uwekezaji. Juhuzi za hivi karibuni za serikali ya CCM za kujaribu kuua utawala wa sharia ni juhudi ovu za kuua uchumi wa nchi yetu. TUZIKATAE juhudi za kuua utawala wa sheria kwa kuwa zitaangamiza taifa letu kiuchumi, kisiasa na kijamii.


Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mb

Kiongozi wa Chama
Dar es Salaam, 
Jumanne 6 Septemba 2016.
Continue Reading...
 

MAISHA TM Copyright © 2012 Template Designed by BTDesigner Published..Blogger Templates· Powered by Blogger